Latest

MASOMO YA MISA, OKTOBA 1, 2017 DOMINIKA YA 26 YA MWAKA A MWANZO: Dan. 3:31, 29, 30, 43, 42 Ee Bwana, yote uliyotutendea, umeyatenda kwa haki, kwa kuwa sisi tumetenda dhambi, wala hatukuzitii amri zako. Ulitukuze jina lako na kututendea sawasawa na wingi wa huruma zako. SOMO 1 Eze. 18:25-28 Bwana ameniambia hivi: Ninyi mwasema, Njia ya Bwana si sawa. Sikiliza sasa, Enyi nyumba ya Israeli; Je! Njia yangu siyo iliyo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa? Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, atakufa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa. Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai. Kwa sababu atafakati, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika, ataishi, hatakufa. Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu. WIMBO WA KATIKATI Zab. 25:4-9, (K) 6 (K) Kumbuka rehema zako, Ee Bwana. Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako; Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha: Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu. (K) Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako. Maana zimekuwako tokea zamani. Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala mausi yangu, Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana, kwa ajili ya wema wako. (K) Bwana yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha njia wenye dhambi. Wenye upole atawaongoza katika hukumu. Wenye upole atawafundisha njia yake. (K) SOMO 2 Flp. 2:1-11 Ikiwako faraja yoyote katika Kristo, yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi, ukiwako ushirika wowote wa Roho, ikiwako huruma yoyote na rehema, ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo yaw engine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. Neno la Bwana…Tumshukuru Mungu. SHANGILIO Yn. 15:15 Aleluya, aleluya Ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Aleluya. INJILI Mt. 21:28-32 Yesu aliwaambia wakuu wa makuhani na wazee, Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. Akajibu akasema, naenda, Bwana; asiende. Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Bwana Yesu akawaambia, Amin, nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini; nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini. Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

MASOMO YA MISA, OKTOBA 1, 2017 DOMINIKA YA 26 YA MWAKA A MWANZO: Dan. 3:31, 29, 30, 43, 42 Ee Bwana,...

MASOMO YA JUMAPILI OCTOBER 1

MASOMO YA MISA, OKTOBA 1, 2017 DOMINIKA YA 26 YA MWAKA A MWANZO: Dan. 3:31, 29, 30, 43, 42 Ee Bwana,...

MASOMO YA MISA JUMANNE.

MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 26, 2017 JUMANNE, JUMA LA 25 LA MWAKA SOMO 1 Ezr. 6:7-8, 12, 14-20 Mfalme...

TAFAKARI YA LEO JUMATATU

“ASLI ITOKAYO MWAMBANI” Tafakari ya kila siku Jumatatu, Septemba 25, 2017. Juma la 25 la mwaka Ezra...

MASOMO YA JUMATATU.

MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 25, 2017 JUMATATU, JUMA LA 25 LA MWAKA SOMO 1 Ezr. 1:1-6 Ilikuwa katika...

MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 24, 2017 DOMINIKA YA 25 YA MWAKA A MWANZO: Bwana asema: Mimi ni wokovu wa...

MASOMO YA DOMINIKA YA LEO.

MASOMO YA MISA,* JUMAPILI, SEPTEMBA 17, 2017 JUMA LA 24 LA MWAKA ________ MWANZO YbS 36:15.16 Ee...
Page 1 of 41234Next
 
Copyright ©2017 CATHOLIC FAITH GROUP • All Rights Reserved.
Design by innocent