TAFAKARI YA LEO JUMATATU

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
“ASLI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Septemba 25, 2017.
Juma la 25 la mwaka

Ezra 1: 1-6;
Zab 126;
Lk 8:16-18

WEWE NI NURU: ANGAZA

Wakati jua linapo zama na giza kuingia, mwanga unaleta tena maisha, na kunakuwa na mizunguko mingine na kazi huendelea. Yesu leo analiweka wazi, kumwamini yeye na kumfuata haipaswi kuwa na moyo nusu nusu na haipaswi kuwa kitu cha “siri” kwamba unakuwa unaona aibu kwasababu ya wengine. Kama wanafunzi wa Yesu hatupaswi kuwa na wasi wasi wowote au kuogopa wengine wanasema nini juu yetu. Hata hivyo, tunatafuta Amani, upendo, msamaha, haki na thamani ya Injili; tunapaswa kutembea tukiwa na ujasiri wote. Tujiringie kuwa wabebaji wa mwanga mkuu-YESU. Haijalishi tutapita katika giza lipi, ulimwengu wenye mashaka, sisi tunao mwanga wenye kuangaza njia zetu mpaka mwisho. Inaweza kuwa ngumu lakini tunapaswa kutembea katika mwanga huu tukifanya kazi na kusonga mbele. Mpaka pale tutakapo kuwa na mwanga huu milele, tusiogope na wala tusipoteze tumaini la mema tutakayo pata kwa hili.

Ukweli huu halisi ni chanzo cha mangamuzi yetu kuhusu uhusiano wetu na Kristo. Katika kweli kama Yesu yupo kweli katika maisha yetu, kama tunaishi maisha ya upendo wa kweli naye, tutaweza kuona matokeo kwa wale tunao ishi nao karibu yetu. Tutaweza kuona mwanga ukiwaangazia wengine. Matokeo ya Yesu kuangaza kupitia sisi itakuwa kama kioo kwa mioyo yetu.

Angalia. Kama watu wanavutwa na upendo wa Kristo kupitia wewe. Kama sio, angalia ndani ya moyo wako na washa tena moto wa upendo wa Mungu . Tufurahi kwamba sisi tunabeba mwanga mkubwa-Yesu. Ulimwengu wenye giza unahitaji mwanga wa Kristo.

Sala: Bwana, njoo washa ndani mwangu, uweke moyo wangu kwenye mapendo kwa upendo wako. Ninatamani moyo wangu uwe chemchemi ya kuwavuta watu kwako. Bwana nitumie mimi kama upendavyo. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
 
Copyright ©2017 CATHOLIC FAITH GROUP • All Rights Reserved.
Design by innocent