TAFAKARI YA LEO ALHAMIS KUTUKUKA KWA MSALABA.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi, Septemba 14, 2017,
Juma la 23, la Mwaka wa Kanisa

Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu

Hes 21: 4-9
Zab 77: 1-2, 34-38
Fil 2: 6-11
Yn 3: 13-17

MSALABA WA KRISTO NI TUMAINI NA UKOMBOZI WETU!

Msalaba ni ishara ya Mkristo. Kila Mkristo, mtoto na hata mtakatifu mkubwa kabisa, wanafanya ishara ya Msalaba, kutoa ushuhuda wa nguvu yake na umuhimu wake. Yesu alitoa maisha yake Msalabani na hapo akakomboa ubinadamu. Kwa njia hii hamna tena alama ya mateso na aibu, bali ukombozi. Msalaba ni njia ya kwenda kwenye utukufu, kwahiyo ni changamoto kwa kila Mkristo. Kama Mtakatifu Paulo anavyosema “Tunamuhubiri Yesu Msulubiwa, kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuuzi, bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani ni Kristo, Nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu” (1 Kor 1: 23-24).

Katika historia ya Ukristo Msalaba aliofia Kristo na kwa njia hii akafufuka, umekuwa ni ishara wazi ya nguvu ya Mungu ya kuokoa. Mababa wa Kanisa wanalinganisha Msalaba wa Yesu na mti wa uzima katika bustani ya dunia, safina ya Noah, na kuni alizobeba Isaka katika mlima Moriah, na ile ngazi ya Yakobo, na ile Fimbo ya Musa, na yule nyoka ya Shaba. Haya yote katika hali ya juu yana husishwa na fumbo la ukombozi. Katika Ubatizo kila Mkristo amesulubiwa na Kristo, kufa na kufufuka na Kristo. Mtakatifu Leo Mkuu anasema, “Msalaba ni chanzo cha kila Baraka, chanzo cha mafanikio yote: kwa waamini unawapa nguvu kutoka katika udhaifu wake, utukufu kutoka katika aibu yake, na uzima kutoka katika kifo”.

Tafakari leo, juu ya msalaba wa Yesu Kristo. Chukua muda Fulani ukiutazama na kutafakari. Na ona jibu katika msalaba huo juu ya shughuli zako za kila siku. Yesu yupo karibu na wale wanaoteseka, na nguvu yake ipo kwa wale wote wanao mwamini ndani yake.

Sala: Bwana, nisaidie mimi niweze kutazama msalaba wako. Nisaidie niweze kuonja ushindi wa mwisho wa mateso yako. Ninaomba nikusanywe na kuponywa ninapo kutazama wewe. Yesu nakuamini wewe. Amina

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
 
Copyright ©2017 CATHOLIC FAITH GROUP • All Rights Reserved.
Design by innocent