KUMBUKUMBU YA LEO KATIKA KANISA.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
14 Septemba kutukuzwa kwa msalaba mtakatifu

Sisi wakristo hatuna budi kuutukuza msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa sababu kwa njia yake ndipo tumekombolewa. Na hivyo ndiyo dhamiri ya sikukuu ya leo. Ushindi na ukuu wa msalaba wake Bwana. Tuyasome maneno yaliyoandikwa kwa Mt. Paulo katika barua zake kwa wakristo.

Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri habari njema tena, nilihubiri bila kutegemeza maarifa ya hotuba za watu kusudi nguvu ya kio cha Kristo msalabani isibatilishwe. Maana ujumbe kuhusu kifo cha Kristo msalabani ni jambo la kipumbavu kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi tulio katika njia ya wakovu ujumbe huo ni nguvu ya Mungu. (1Kor.1:17-18)

“Mimi sitajivunia kamwe chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo maana kwa njia ya msalaba huo ulimwengu umesubiliwa kwangu nami nimesulubiwa kwa ulimwengu.” (Gal.6:14)

Kristo mwenyewe ametuletea amani kwa kuwafanya wayahudi na watu wa mataifa mengine kuwa jamii moja. Kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja, na kuzipatanisha na Mungu. (efe.2:14-16)

“Alijinyenyekeza na kutii mpaka kufa, hata kufa msalababi wako watu wengi ambao ni adui wa msalaba wa Kristo.

Mwisho wao ni motoni, kwani tumbo lao ndio mungu wao. Wanaona fahari juu ya mambo ya kidunia. Lakini sisi ni raia wa mbinguni, na twatazama kwa hamu kubwa Mkombozi aje kutoka mbinguni. Bwana Yesu Kristo. Yeye ataibadili miili yetu dhaifu inayokufa na kuifanya ifanane na mwili wake mtukufu kwa nguvu ile ambayo kwayo anaweza kuviweka vitu vyote chini ya Utawala wake” (Fil.2:8 na 3:18-21)

“Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea, yeye alivumilia kifo msalabani, bila kujali juu ya aibu yake, na sasa anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.” (Ebr.12.2)

Tunautukuza Msalaba ambao ni juu yake Kristo aliyetukomboa kutoka kwa dhambi. Kutukuzwa kwa Msalaba adharani kulianzia karne ya 4, baada ya kugunduliwa kwa Msalaba Mtakatifu na Malkia Mtakatifu Helena, Mama wa Constantino mfalme, wakati Helena alihiji Jerusalemu. Kwenye hija hiyo, makanisa mawili ya Jerusalemu yalifunguliwa rasmi na Mfalme Constantino, na siku hio hio Msalaba Mtakatifu ukagunduliwa na Helena. Siku kuu yenyewe yakumbuka ushindaji wa Msalaba au kutokea kwa Msalaba katika nuru. Wayahudi walinung’unika mbele ya Mungu kwa kuwa Mungu aliwapatia chakula cha jangwani. Hivyo wakamkosea Mungu. Basi ili kuwatesa, Mungu akawatumia nyoka zenye sumu kali, na wengi wao wakafa kwa kuumwa na nyoka hao. Basi walipogeuza mioyo yao, Mungu akamwambia Musa atundike mfano wa nyoka wa shaba ya chuma juu ya mti. Wale walioumwa na nyoka wakiangalia ule mfano wa nyoka wa shaba juu ya mti walipona. Mfano huo wa nyoka wa shaba juu ya mti mrefu ulikuwa mfano wa msalaba wa Kristo. Naye Paulo kwenye Waraka wake kwa Wafilipi atuambia kwamba Yesu "alikubali kuacha vyote, akachukua hali ya mtumishi, akazaliwa na umbo la wanadamu. Alipochukua umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii mpaka kufa, tena kifo cha msalaba… Kwa sababu hiyo, Mungu alimwinua juu kabisa, akampa jina ambalo ni kuu kuliko majina yote.”

Mungu alikuwa amemwambia Musa ainue ule mfano wa nyoka wa shaba juu ya mti. Wale walioangalia ule mfano wa nyoka wa shaba juu ya mti baada ya kuumwa, walipona. Basi Msalaba wa Yesu ndio ungeweza kutuponya. Ule mfano wa nyoka wa shaba juu ya mti mrefu ulikuwa pia mfano wa Msalaba wa Yesu. Msalaba ni mfano wa ukombozi wetu, yaani mateso, kufa Msalabani na kufufuka. Wakristo wautukuza Msalaba Mtakatifu wa Kristo kama msing wa imani na chombo cha ukombozi. Tunautumia Msalaba pia kwa kuuweka ndani ya kanisa au nyumbani, au kwenye mashule yetu na nyumba. Basi tuombe ili kwa ushindi huo wa Kristo hata sisi kwa ushuhuda wetu, tupate kushinda upinzani uliopo kuhusu Msalaba wa Yesu kama msing wa imani yetu na chombo cha ukombozi wetu. ”Tunakuabudu Ee Kristo na tunakuheshimu, kwa maana kwa kifo chako Masalabani umeukomboa ulimwengu”.


NB: SALA MBELE YA MSALABA
 (sala iliyokutwa kwenye kaburi la yesu 1503 AD)
Ee Mungu mwenyezi uliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu,uwe nami. Msalaba Mtakatifu wa Yesu-unihurumie. Msalaba Mtakatifu wa Yesu-uwe mkingaji wangu Msalaba Mtakatifu wa Yesu-uniondolee maovu yote. Msalaba Mtakatifu wa Yesu uniondolee maumivu yote. Msalaba Mtakatifu wa Yesu-unifanye niende kwenye wokovu. Unikinge na ajali za mwili,uniondolee hatari ya kifo cha ghafla.Nauabudu msalaba mtakatifu wa Yesu Kristu wa Nazareti uliyesulibiwa,unihurumie, unifanye niweze kuondokana na Roho ya uovu wakati wote, Ee mama wa msaada wa daima, naja mbele ya picha yako takatifu, na kuomba msaada wako kama mtoto.

Jioneshe sasa kwangu kwamba u mama unionee huruma. Ee mama mpenzi wa msaada wa daima,kwa ajili ya upendo uliokuwa nao kwa Yesu na kwa heshima ya majeraha yake matakatifu, unisaidie haja yangu......(taja). Ee mama mpendevu,ninayaacha yote kwako kwa Jina la Baba,ninayaacha yote kwako kwa Jina la |Mwana,ninayaacha yote kwako kwa Jina la Roho Mtakatifu.Amina

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
 
Copyright ©2017 CATHOLIC FAITH GROUP • All Rights Reserved.
Design by innocent